Monday, July 13, 2015

Hatimaye kiungo wa Southampton, Morgan Schneiderlin amekamilisha vipimo tayari kujiunga na Manchester United wiki hii.
Schneiderlin ambaye alikua akiwaniwa na klabu za Arsenal, Manchester United na Tottenham Hotspur, amefikia tamati baada ya kutua Carrington uwanja wa mazoezi wa United, kufanyiwa vipimo tayari kwa kuuvaa uzi wa klabu hiyo.

Schneiderlin mwenye miaka 25 alikua kiungo wa pili nyuma ya kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic kwa 'tackling' nyingi msimu uliopita.

Morgan Schneiderlin, raia wa Ufaransa atakua ametimiza ndoto zake za kucheza klabu bingwa Ulaya, kwani ndicho kilichomuondoa Soton.

Awali Southampton walikataa ofa ya pauni 20m kutoka kwa Manchester United, kwa kuwa wanaamini thamani ya kiungo huyo mkabaji ni zaidi ya pauni 25m.

Aidha huo ni usajili wa nne wa klabu hiyo ya Manchester msimu huu mara baada ya kuwanasa tayari, Memphis Depay, Matteu Darmian na Bastian Schweinsteiger.


Wakati huo huo imeelezwa kuwa bado Manchester United inasaka saini ya mlinzi wa Real Madrid, Sergio Ramos ili wakamilishe usajili wao.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video