Tuesday, July 28, 2015

Timu ya Gor Mahia ya Kenya imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kagame Cup baada ya kuitandika Malakia FC ya Sudan Kusini kwa goli 2-1, kwenye mchezo wa robo fainali uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa.
Godfrey Walusimbi amefunga magoli yote mawili ya Gor Mahia na kuivusha timu hiyo hadi kwenye hatua ya nusu fainali. Ilichukua dakika mbili tu Gor Mahia kuandika goli la kwanza lililofungwa na mashambuliaji raia wa Uganda Godfrey Walusimbi kabla ya kufunga goli lingine dakika ya 27 kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Malakia walionekana kucheza kwa nguvu na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara wakitafuta goli ambapo walifanikiwa kupata goli la kufutia machozi kupitia kwa Thomas Jacob Mathew. Kipindi cha pili Gor Mahia ilionekana kuridhika na matokeo ya kipindi cha kwanza kwa kucheza mpira wa taratibu wakionekana hawahitaji tena kufunga goli

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video