Kamati ya uendeshaji wa michuano ya CEKAFA ya hapa nchini (Local Organization Committee) iliwasilisha malalamiko yake kwa CECAFA kutokana na utovu wa nidhamu uliooneshwa na kocha wa timu ya Gor Mahia Frank Nuttal pamoja na timu yake kwa ujumla kwa kuingia uwanjani kupitia mlango ambao haukupaswa kutumiwa na timu hiyo wakati inaingia na kutoka kwenye vyumba vya kuvalia.
Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto amesema, baada ya malalamiko hayo, jana CECAFA imeiandikia barua timu ya Gor Mahia ya kuwapa onyo kali juu ya tabia na vitendo vilivooneshwa na timu hiyo havipaswi kuoneshwa wala kurudiwa na katika mihezo inayokuja ikihusisha timu yao.
“Gor Mahia wameambiwa endapo wataendelea kutenda kosa hilo, basi hatua nyingine zitachukuliwa. Lakini kwenye mchezo wa jana waliweza kufata taratibu ambazo zimewekwa kwa ajili ya matumizi ya uwanja wetu wa Taifa”, amesema Kizuguto.
0 comments:
Post a Comment