Friday, July 10, 2015


Na Ramadhani Ngoda.
Nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard ameamua ‘kumchana makavu’ nyota wa klabu hiyo anayeuumiza kichwa uongozi wa Liverpool Raheem Sterling na kumwambia awe ‘mwanaume’ na kuwa na msimamo juu ya mstakabali wake Anfield.
Sterling ambaye kwa sasa amerejea mazoezini baada ya kukosekana kwa siku mbili ikidaiwa kushinikiza klabu hiyo kumuuza ilihali majogoo hao wa jiji bado wanahitaji huduma ya mzawa huyo wa Jamaica.

Ktika mahojiano maalumu na sky sports makao makuu, Gerrard amesikitishwa na tabia chafu ya winga huyo na kukiona kitendo hicho kuwa si cha kiungwana kwa wapenzi wa klabu hiyo walioonesha kumthamini na kumpenda kipindi chote cha maisha yake Liverpool.

“Raheem anatakiwa aingie ndani na aongee na wamiliki wa klabu na Brendan (Rodgers) mwenyewe, awaeleze nini anataka,” alisema Gerrard.

“Kuna mamilioni na mamilioni ya mashabiki wa Liverpool duniani  kote wanaopenda kumuona Raheem akiwa kwenye jezi ya Liverpool. Hivyo sidhani kama ni vizuri kwao kusikia anafanya vitu kama hivi,” aliongeza nahodha huyo wa zamani wa Liverpool.

Kuonesha bado Liverpool inamuhitaji Sterling, tayari miamba hiyo ya England imeshakataa ofay a Manchester City ya pauni milioni 40 kutoka kwa matajiri wa jiji la Manchester, Manchester City.

Licha ya Sterling mwenyewe kukiri kuwa yeye hasukumwi na pesa katika maamuzi yake, bado wakala wake Aidy Ward alishasema kuwa Raheem asingesaini mkataba mpya na Liverpool hata kama ungemlipa pauni 900,000 kwa wiki.



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video