Friday, July 31, 2015

Mfungaji wa goli la Azam FC Shah Farid Mussa (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake wa Azam mara baada ya kuigungia timu yake goli lililoivusha mpaka hatua ya fainali
Azam FC ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya Kagame Cup wafanikiwa kutinga fainali ya mashindano hayo baada ya kuilaza KCCA ya Uanda kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa nsu fainali uliomalizika jioni ya leo kwenye dimba la Taifa.
Goli pekee la Azam limefungwa na Shah Farid Mussa dakika ya 76 kipindi cha pili na kuihakikishia Azam kucheza fainali ya Kagame kwa mwaka 2015.
Kipindi cha kwanza kilimalizika huku timu hizo zikienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana (1-1) lakini timu zote zikiwa zimepoteza nafasi za kufunga kwenye kipindi cha kwanza. Jonh Bocco na Kipre Tchetche kila mmoja alikosa nafasi ya kufunga kwa wakati wake baada ya Azam kufanya mashambulizi mawili ambayo yalikuwa ni makali.
Sserunkuma Isaac wa KCCA nae alikosa goli baada ya kipa wa Azsam FC Aishi Manula Salum kuokoa mpira uliokuwa unaelekea golini kabla hajapumzishwa kumpisha Kondo Shaban mabadiliko ambayo yalifanywa ndani ya kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili Azam walianza kwa kufanya mabadiliko ambapo walimpumzisha Mudathir Yahya na nafasi yake ikachukuliwa na Ame Ally ‘Zungu’ na baadae akaingia Shomari Kapombe huku Erasto Nyoni akienda kwenye benchi na Kipre Tchetche akatolewa kumpisha
Mwanzoni mwa kipindi cha pili, KCCA ilifanya mashambulizi kadhaa golini kwa Azam lakini uimara wa ukuta wa Azam uliweza kuhimili kashikashi hizo.Huku KCCA wakionekana kutawala mchezo katika eneo la katikati na kucheza mipira mirefu hali iliyowapa ugumu Azam.
Kadiri muda ulivyokuwa ukiyoyoma Azam walionekana kuelemewa kwani Manula alifanya kazi ya ziada kuokoa kombora la Ochaya Joseph alilopiga akiwa nje ya eneo la mita 18.
Baada ya Azam kupata goli, KCCA walifanya mabadiliko kwa kumpumzisha Habibu Kavuma na kumuingiza Birungi Michael lakini bado mabadiliko hayo hayakuzaa matunda kwa upande wao kwani hadi filimbi ya mwisho ya mwamuzi Souleiman Ahmed kutoka Djibouti Azam waliweza kutoka uwanjani wakiwa mbele kwa goli 1-0 na kutinga fainali ya Kagame kwa mara ya pili katika hisoria yao
Azam sasa watacheza na Gor Mahia ya Kenya kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwwa kuchezwa siku ya Jumapili. Gor Mahia walifuzu kucheza fainali baada ya kuifunga Khartoum ya Sudan kwa goli 3-1 kwenye mchezo uliotangulia mchana wa leo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video