Bondia Floyd 'money' Mayweather maarufu kama 'The Best Ever' anatarajiwa kurudi tena ulingoni September 12 mwaka huu mara baada ya pambano lake la May 3 alipomshinda Manny Pacquiao kwa pointi.
Awali kulikuwa na sintofahamu ya kama Floyd anaweza kucheza tena mara baada ya pambano lake na seneta wa Ufilipino, Manny Pacquiao, lakini sasa atapigana, imefahamika.
Bondia huyo mwenye 'mawe' wiki hii ali*post video katika ukurasa wake wa Instagram, akionesha akifanya mazoezi mazito huku akiandika kuwa ni maandalizi ya pambano lake la September 12 mwaka huu.
Lakini swali hapa ni nani atapigana nae? Hakuna uwezekano wa kurudiana na Manny Pacquiao kutokana na wawili hao kutokuwa na maelewano mazuri kutokana na Mayweather kukasirishwa na visingizio vya Pacquiao kwamba alikua mgonjwa wa bega katika pambano lao la may mwaka huu.
Aidha bondia wa Uingereza, Amir Khan amekua mara kwa mara akijinadi kumtaka Floyd ulingoni.
Hata hivyo haijathibitika ni nani atapigana na bondia huyo ambaye ndiye mwanamichezo mwenye pesa nyingi kuliko wote duniani.
Hata hivyo inasubiriwa kuona kama Mayweather atakusanya mtonyo mkubwa kama ilivyokuwa awali dhidi ya Pacquiao walipooingiza dola 300m za marekani katika usiku mmoja na kufanya pambano lao kuwa tajiri zaidi katika historia ya ngumi duniani.
0 comments:
Post a Comment