Tuesday, July 21, 2015

Kwa mara ya pili, Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limeiamuru klabu ya Simba SC kulipa fidia ya kuvunja mkataba na beki wake wa zamani, Mkenya, Donald Mosoti Omanwa
Simba walivunja mkataba wa Mosoti Agosti 2014 bila matakwa ya mchezaji.
Taarifa kutoka Kenya zinaeleza kwamba, Simba wanatakiwa kumlipa Mosoti kufikia Jumatatu ya Julai 27 na wakishindwa kufanya hivyo, keshi hiyo itapelekwa kamati ya nidhamu ya FIFA.
Simba walivunja mkataba wa Mosoti akiwa amebakiza mwaka mmoja na miezi mitatu na kutokana na hali hiyo mlinzi huyo alipeleka kesi FIFA kupitia kwa mwanasheria wake,  Felix Majani.

AMRI YA KULIPA
Baada ya FIFA kusikiliza pande zote mwezi Februari mwaka huu, waliamuru Simba imlipe fidia Mosoti ndani ya siku 30 kutoka siku ya maamuzi.
Majaji waliofanya maamuzi hayo ni Thomas Grimm (Switzerland), Eirik Monsen (Norway) na Zola Majavu (Afrika kusini)  na walisema Simba wakishindwa kulipa hadi siku ya Deadline,  watafikisha kesi kamati ya nidhamu.
 Baraza la Sheria na hadhi za wachezaji la FIFA chini ya kiongozi wake, Sarah Solemale, limesema kuwa Simba waliandika barua ya kukata rufaa Alhamisi ya Julai 16 mwaka 2013, lakini haikufuata taratibu, hivyo Desemba 12 mwaka 2013 wakaiamuru imlipe Mosoti fidia ya Dola 13, 800, lakini haijafanya hivyo mpaka leo.
Simba ikikamilisha malipo hayo inatakiwa kupeleka FIFA nakala ya risti ya malipo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video