Habari za wakati huu wapenzi wa michezo hususani wale wa tathnia pendwa ya mpira wa miguu maarufu kama soka. Binafsi mimi ni mpenzi wa muziki wa kufoka foka ambao kule kwenye nchi yenye maandishi matatu wanauita "Hip Hop".
Mnamo mwezi Mei kuna kijana mmoja nilikuwa namuona kwenye mtandao wa "You Tube" kama "Rapa" anaelekea Kaskazini Magharibi mwa England katika jiji la Manchester kwenda kukamilisha usajili wake kutoka pale Uholanzi katika klabu ya PSV Eindhoven.
Sikuupenda usajili huu maana huyu Rapa kwenye soka ni hatari sana, naamini kwa sisi ambao tunaichukia United, msimu ujao hatuna chetu tena...
Mpaka sasa bado sijakwambia ni nani ambaye namkusudia hapa, ila kwa wale wajanja tayari wameshamgundua ni nani hasa ambaye namzungumzia hapa.
Huyu ni kijana mdogo ambaye kimwonekano lazima utakubaliana na mimi kuwa endapo angezaliwa "Bongo" bila shaka angekuwa makamu wa raisi wa "WCB Wasafi" lakini vijana wa kileo wanamuita "Handsome".... Hapa namzungumzia Memphis Depay, kiungo mshambuliaji anaependa kutokea kushoto, itakuwa vyema kama tukikaa wote hadi mwisho wa makala hii ili tujadili mchango wa kinda huyu msimu ujao kwenye timu ya Manchester United, klabu ambayo imepania kurudisha heshima yake tena...
Bila shaka utakubaliana na mimi kuwa tangu aondoke Mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea pale Man U, Christiano Ronaldo, hakuna Mchezaji mwingine ambaye ameendeleza "Dribbling" na kupiga mipira iliyokufa kama alivyokuwa anafanya Cr7, pia wachezaji ambao wanapenda kucheza
mipira mirefu kwa wakati muafaka pale panapohitajika hawakuwa vizuri, nadhani unakumbuka baadhi ya mechi ambazo Man U walifanya vibaya kuna baadhi ya vitu vilikosekana, nitakuona mzushi kama utasingizia mfumo
wa van Gaal, japokuwa "sometimes" mifumo inachangia ila mara nyingi sana kunakosekana Wachezaji muafaka katika wakati muafaka...
Sasa kwa heshima na taadhima naomba tuangalie mapungufu ya Man U msimu ulopita japo kwa uchache, licha ya kuwa na Washambuliaji wazoefu,
United ilifunga jumla ya magoli 71, licha ya kuwa na watu wenye kasi na uwezo wa kupiga vyenga kuelekea kwenye lango la wapinzani bado "Top scorer" wa United alikuwa na jumla ya magoli 14, tena huyu hakua winga wala mshambuliaji, mara nyingi alikuwa anacheza kama kiungo huku akitumia muda mwingi kukaba na kuanzisha ama kuendeleza mashambulizi, hapa nazumngumzia Wayne Rooney. Hata ukijaribu kuangalia mipira iliyokufa, mara nyingi United ilionekana kufanya vibaya....
Bila shaka usajili wa di Maria ulikuwa ni kuja kuhakikisha United inarudisha makali yake ya kuwa na Mawinga hatari kabisa duniani kama walivyokuwa akina Cr7, David Beckam ama Cantona, ila hali haikuwa hivyo.
Ukiachilia mbali mapungufu haya machache, binafsi naamini kuna
mtu sahihi katua Man U katika majira haya ya usajili huyu sio mwingine bali ni Depay. Bila shaka mabeki wa Epl wajiandae msimu ujao kwani inawezekana safari ya Depay kuwa kwenye level za akina Eden Hazard ikaanzia pale Old Trafford, unajua kwanini nasema hivi, em tumuangalie
uwanjani huwa anafanya nini..!!
Huyu "Dogo" ni mwepesi sana na anapenda kutokea kushoto na mara nyingi sana ni mgumu kupoteza mipira ovyo kama akina fulani!! anapenda sana kuwafata mabeki pindi akiwa na mpira huku mara nyingi pia anaingia ndani na hii itasaidia kuwafungua mabeki na kama United watapata
Mshambuliaji mzuri ambaye atakuwa "Clinical finisher" mzuri, basi bila shaka hapa ndo magoli mengi yatapatikana. Kumbuka pia wale mabeki wa
pembeni na wa kati ambao wamezoea kucheza faulo kibao wanapaswa kuwa makini kwani Depay anaweza kupiga "Free kick" kwa ustadi mkubwa..! natamani sana Mungu atupe uhai tuone ujuzi wa Depay msimu ujao.
Kama unakumbuka di Maria na Mata walifunga goli moja moja kwenye mipira iliyokufa msimu ulopita, ila naamini Depay anaenda kuwa "Mtamu" zaidi ya "Mcharo" katika mipira hii, pia jamaa naamini anakwenda kutoa
"assist" za kutosha kwa Wafungaji pale United, hii ni kwasababu Depay ni mjuzi wa pasi sana hasa akiwa eneo la hatari ambalo mara nyingi wachezaji kibao wanashindwa kufanya maamuzi katika eneo hili. Ngoja tusubiri mfumo wa van Gaal lakini naamini mfumo wowote atakao utumia
atahakikisha Depay anafiti kwani tayari walishawahi kufanya kazi pamoja. Pia miguu yake na kichwa chake kitainufaisha sana Man U.
Kwa lugha ya Kiarabu tunasema "In shaa allah" yaani "If God Will" kwa kimombo, ila huku uswahili tunasema Mungu akipenda tutamuona Depay akienda kuwasumbua mabeki hasa wale pembeni, naamini atafanya makubwa
kwani kule Uholanzi kawapiku hata Washambuliaji wa kati, pia naiona tuzo ya mchezaji bora chipukizi ikienda kwa Depay msimu ujao, naamini United inaenda kumtengeneza Winga hatari kabisa kuwahi kutokea Uholanzi, pia namuona Depay akivuka bahari hadi USA kwenda kufanya
"collabo" na akina Jay Z baada ya kutengeneza jina lake mara nyingine pale United, kila lakheri Bwana mdogo Depay.
0 comments:
Post a Comment