Friday, July 10, 2015

MSANII wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo Fleva’ na Filamu nchini, Hamis Ramadhani Baba Maarufu kama  H Baba anaendelea kufanya majaribio ya kucheza soka katika klabu mpya iliyopanda ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao, Toto Africa ya Mwanza.
H Baba amefanya mahojiano maalum na mtandao huu na kueleza mengi kuhusu kipaji chake cha soka, muziki na filamu na namna anavyoendelea na majaribio katika klabu hiyo ya mitaa ya kishamapanda.
Fuatilia mahojiano hayo hapa chini;
Swali: Majaribio yako ya kucheza soka Toto Africa yanakwendaje?
H Baba: Naendelea vizuri, kikubwa ni kwamba,  nafanya mazoezi saa 9,  nakutana na wenzangu saa 10 jioni. Mpira hauhitaji maneno, unahitaji mazoezi. Nafanyishwa mazoezi binafsi saa 9 alasiri kwasababu nimekaa kipindi kirefu bila kucheza mpira, mambo yanakwenda Fresh, hapa ‘Control’ zipo, kupiga mashine golini kama kawaida, sasa lazima niwe na pumzi, ndio maana naanza mazoezi mapema chini ya kocha msaidizi, Almasi.
h2
Swali:  Watu wengi wamekufahamu kupitia muziki, historia yako katika mchezo wa soka ikoje?
H Baba: Nimecheza timu nyingi sana kabla ya kuimba muziki, nilishacheza sana kwasababu nilikuwa katika hali ya utafutaji, nilicheza timu kama Mabatini United, Nyashala ya Jeshi, Polisi ya Mabatini, Kombaini ya Mabatini, Pamba, nikaenda Toto ambapo pesa ya usajili nilikuja kutengeneza wimbo wa ‘Mpenzi wangu Bubu” , baada ya hapo nikaacha mpira, nikaingia kwenye muziki.
2009 nikaenda Azam fc kufanya majaribio, tulikuwa tunacheza pale Pugu, John Bocco namba 10 mimi nacheza namba 9, lakini nikaacha na kuendelea na mambo yangu ya muziki.
h3
Swali: kwasasa  unajiona uko tayari kucheza soka au unajaribu tu?
H Baba: Kwasasa hivi sijaribu, nataka kuonesha namna gani H Baba anaweza kandanda ambayo haihitaji maneno. Mtu akisema nimuhadithie kuhusu mpira naweza kutumia kipindi kizima, nimecheza timu nyingi sana, hii kanda ya ziwa wananijua sana, Pamba, Toto kote nilishavuruga.
Sasa hivi nimeamua nicheze mpira, pia nina Albamu yangu mpya inakuja, mashabiki wangu siwezi kuwaacha hivi hivi, nawapa burudani kama kawaida, Show nitapiga kama kawaida, filamu nitatoa kama kawaida.
Lengo ni kuwafundisha vijana kwamba sanaa zote zinafanana, ukiamua kucheza mpira sio kwamba uache muziki, unaweza kufanya vyote, sanaa zote zinafanana, ni wewe tu ku-balance muda wako na kufanya mazoezi na kupunguzu starehe.
h4
Swali: Unaonekana kuwa na vipaji vingi,  kipi unakipenda zaidi?
H Baba: Napenda vyote, mimi kama sikipendi kitu sitati hata kushiriki na sipendi kujifunza. Mimi napenda muziki, soka na filamu ambazo zinaniingizia hela. Ni kazi zinazonipa hela, heshima, nimeoa, nina mke na watoto wawili, ni kitu cha kujivunia. Kuna wasanii wengi hawana watoto, hawajui hata lini wataoa. Mimi nimeweza kwasababu ya sanaa.
Swali: Wachezaji gani wakubwa umewahi kucheza nao?
H Baba: Nimecheza na Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Shamte Ally, wachezaji kibao nimecheza nao. Ninachoangalia sasa nifanye nini ili nioneshe kipaji changu, sio kila mtu amepewa vipaji vingi, wengine wameishia fani moja tu. Mimi ni fundi wa mpira, ni fundi wa muziki, watu wote wanajua, hata kama nitakuwa nacheza mpira, hakuna msanii yeyote atayenifikia kutawala jukwaa, wengine wanategemea wacheza show, mimi najitegemea mwenyewe.
Nilishaweka mpambano, msanii ambaye wanamwaminia sana kwamba  ni mkali na anawezasana Jukwaani, muiteni tufanye show, yeye alipwe, mimi nafanya bure, mwaka watatu hajajitokeza mtu, natafuta kila siku.
h1
Swali: Mke wako Flora Mvungi ni mtu wa filamu, amechukuliaje maamuzi yako ya kuingia miguu yote kwenye soka tena ngazi ya ligi kuu?
H Baba: Bado tunavutana naye, yeye hajatoa maamuzi kabisa, lakini kwasababu mimi ni baba mwenye nyumba nilishafanya maamuzi yangu na yeye ana yake, nataka nimshawishi na nitazidi kumshawishi ili aridhie.
Swali: Wale mashabiki wako wa Muziki ambao wanazipenda Simba na Yanga huoni kama watakuchukia ukiwafunga?
H Baba: Naomba wasinilaumu, wasiache kusikiliza nyimbo zangu na wasinichukie, hata watangazaji wanaopenda Simba na Yanga wasiache kupiga nyimbo zangu. Kumfunga Simba, Yanga ni kawaida tu.
Kumuua Simba au Yanga ni dakika moja tu, kama naanza kwenye mechi ujue namuua dakika yoyote, wasije wakanibagua kwasababu nimeifunga Yanga au Simba.
Swali: Kwanini unajiamini kiasi hicho?
H Baba: kwasababu kuna wachezaji wengi hawajawahi kufunga uwanja wa Taifa mkubwa na Shamba la Bibi, mimi kote nilishatandika, nacheka na nyavu sana. Mimi natumia miguu yote, kwa karne hii kumpata mchezaji mwenye umbo kama langu, halafu anapiga miguu yote kwa nguvu sawa ni ngumu sana, ni wachache sana nikiwemo mimi. Hakuna kipa yeyote aliyewahi kudaka penati yangu, natumia miguu yote, kipa kulala kulia mpira kuingia kushoto kawaida yangu. Ndio maana mashabiki wanaokuja CCM Kirumba wanafurahi sana.
Swali: Endapo utafuzu kujiunga na Toto, ukienda kucheza mikoani na kuombwa ufanye Show,  uko tayari?
H Baba: Hapo itakuwa ni baada ya mechi, kabla ya mechi siwezi kufanya shughuli yoyote, kuna wakala anayenisimamiea kwenye soka, nina Menejimenti ya muziki na filamu, kama mtu ananitaka kwenye muziki ataongea na meneja ili tufanye Show baada ya mechi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video