Wednesday, July 22, 2015

Mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye uhamisho wake daima umekuwa ukizungukwa na maswali kila aendako, ameingia katika utata mwingine baada ya ripoti mpya kudai kwamba alisaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea timu ya SønderjyskE licha ya timu hiyo ya Denmark kutotoa hata senti kwa klabu yake ya Simba.
 
Utata huo mpya umefuatia Wadenmark hao kutaka kumrejesha Okwi Simba kwa mkopo wa miezi sita baada ya kukwama kuipata   leseni yake ya uhamisho ya kimataifa (ITC), ambayo Simba imesema haitaitoa hadi itakapolipwa ada ya uhamisho dola 110,000 (sawa na Sh. milioni 220).
 
Kumekuwa na mitazamo kwamba kutolewa kwa mkopo kwa Okwi Simba kunaweza kuwa ni janja ya timu hiyo ya Denmark kuvizia Mganda huyo amalize mkataba wake Msimbazi unaomalizika Mei mwakani ili imchukue bure.
 
Hata hivyo, klabu kubwa kama ya Simba inatarajiwa kwamba ilisaini mkataba na SønderjyskE ambao unaifunga klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Denmark kwamba lazima ilipe deni hilo, hata kama itamleta Msimbazi kwa mkopo.
 
Taarifa nyingine zinasema kuwa klabu hiyo ya Denmark imefikia uamuzi huo baada ya kumnasa mchezaji mwenye kiwango cha juu zaidi ukilinganisha na Okwi na gharama zake za usajili ni za chini.
 
Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema kwamba kwa sasa wao wanachofuatilia ni kuhakikisha wanalipwa kiasi hicho cha fedha ndipo waruhusu usajili wa njia ya mtandao ufanyike.
 
Aveva aliweka wazi kwamba, walimuuza Okwi baada ya mchezaji kuangalia maslahi yake na sasa umefika wakati klabu kuhakikisha inapata haki yake na si kuona makosa yaliyofanyika huko nyuma yanajirudia.
 
Katika uongozi wa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage, Okwi aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel kwa dau la Dola za Marekani 300,000 lakini fedha hizo hazikulipwa hadi leo na baadaye mshambuliaji huyo alirejea klabu yake ya zamani ya SC Villa na muda mfupi alijiunga na Yanga.
 
Mganda huyo aliichezea Yanga katika kipindi kifupi na kurejea Simba kwa kueleza kuwa mabingwa hao wa Tanzania Bara hawakutimiza baadhi ya vipengele vilivyoko kwenye mkataba wake.
CHANZO: MTANDAO WA IPP MEDIA

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video