Friday, July 10, 2015

Klabu ya Sonderjyske ya nchini Denmark imempokea mshambuliaji wake mpya Emmanuel Okwi na kumkabidhi jezi yake namba 25 ambayo alikuwa anaitumia alipokuwa anacheza Simba.
Okwi hajafanya majaribio katika klabu hiyo kama walivyodai Simba bali amesaini mkataba wa kudumu wa miaka minne kwa dau linalosemekana kuwa dola laki tatu na nusu.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Hans Jørgen Haysen amesema, wamekuwa wakimfuatilia Okwi na wamefurahi kumsaini mshambuliaji huyo. “Tumekuwa tunamfuatilia Emanuel Okwi kwa muda sasa, na tumefurahi tumefanikiwa kukubaliana nae, si yeye tu bali hata klabu yake ya zamani Simba SC kwa kukubaliana nasi”, Jørgen aliiambia tovuti ya klabu.
Hans Jørgen amesema, Okwi atatoa mbadala kwenye timu hasa kwenye eneo la ushambuliaji na wanatarajia makubwa kutoka kwake lakini akasema mshambuliaji huyo anaweza akahitaji muda kidogo ili kuendana na soka la Ulaya.
“Tukiwa na Emanuel Okwi, tutakuwa na uwanda mpana wa kucheza vizuri kwenye eneo la ushambuliaji na ni mchezaji ambaye tunatarajia mengi sana kutoka kwake”, Hans Jørgen amesema.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video