Wednesday, July 1, 2015


Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamemsajili kiungo wa Brazil Douglas Costa kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk.
Costa, 24, amejiunga na Bayern kwa dau la pauni milioni 21 kwa mujibu wa klabu yake hiyo ya Ukraine na amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabuya Bayern.
“Ndoto zangu zimetimia leo”, amesema Costa ambaye amerejea kwao na kikosi cha Brazil akitokea kwenye michuano ya Copa America.
Usajili huo utaongeza tetesi za kiungo wa timu hiyo Bastian Schwensteiger kujiunga na Manchester United.
Guardiola ambaye amekiongoza kikosi cha Bayern kutwaa taji la 25 la Bundesliga msimu uliopita, anamachaguo mengi ya viungo akianza na Frank Ribery na Mhispania Thiago Acantara, Xabi Alonso na Javi Martinez, hiyo inamaanisha Schweinsteiger, 30, atakuwa na nafasi ndogo ya kucheza kwenye kikosi hicho.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani, amecheza mechi 20 tu za ligi msimu wa 2014-2015 ambazo ni mechi chache kwake tangu ajiunge na Bayern mwaka 2002.
Costa alifunga magoli 29 kwenye michezo 149 ya ligi ambayo alicheza akiwa Shakhtar ambapo ameshinda mataji mara tano.
“Douglas Costa atakuwa ni mchezaji mzuri kwenye timu yetu”, alisema mkurigenzi wa michezo wa Bayern Mathias Sammer, “Ana uwezo wa ufundi, nguvu hasa mguu wa kushoto, yuko shapu na anakasi”.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video