Kazimoto (kulia) akiwa na Rais wa Simba, Evans Aveva
Hatimaye kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Mwinyi Kazimoto ameendelea kuongeza idadi ya wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kucheza soka la kulipwa na kurejea nchini kuendelea kucheza timu za ligi kuu soka Tanzania bara.
Kiungo huyo ambaye alikuwa anaichezea klabu ya Al Markhiya inayoshiriki ligi kuu ya Qatar tangu mwaka 2013 akitokea klabu ya Simba amerejea tena msimbazi na kusaini mkataba wa miaka miwili mbele ya Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva.
0 comments:
Post a Comment