Makamu bingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam FC wameendelea kujiimarisha wakati huu wa usajili wa majira ya kiangazi baada ya mchana huu kumsainisha Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Kenya, Allan Wanga.
Wanga, mshambuliaji wa zamani wa Al Merrikh ya Sudan amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Mkenya huyo hatasahaulika akilini mwa Azam kwani ndiye aliyeifungia Merreick goli la tatu lililowatupa Azam nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwezi Februari mwaka huu.
Awali Azam walishinda 2-0 Chamazi Dar es salaam na walipokwenda Khartoum, Sudan walikufa 3-0 na goli la tatu lilifungwa na nyota waliyemsajili leo.
0 comments:
Post a Comment