Kocha wa Manchester United ana shauku kubwa ya kusajili mshambuliaji mpya katika dirisha hili la usajili majira ya joto, huku akisisitiza kuwa Mashetani hao Wekundu wanahitaji mtu mwenye uwezo, na kauli hiyo inawezekana ikawa na maana kuwa yuko mbioni kumnyaka Romelu Lukaku, kwa nini?, endelea kusoma hapo chini.
Memphis Depay ameonekana kama amefichua siri ya kocha wake kuhusu usajili wa mshambuliaji huyo kutokana alichoandika katika ukurasa wake wa Instagram.
"Itakuwa ni 'surprise', kwa sababu bado nipo katika mchakato", alisema Mdachi huyo mwanzoni kabisa mwa dirisha la usajili". Sio mshambuliaji ambaye vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikimtaja. Ninyi subirini tu, mtaona".
Na sasa Depay pengine atakuwa ameshaweka kila kitu wazi, mara baada ya kuposti picha yake akiwa pamoja na mshambuliaji wa Everton Lukaku wakifurahia mapumziko yao wakati huu wa maandalizi ya msimu mpya na kundika ujumbe wa kushtua kidogo ambao ulisomeka hivi "see you soon"(tutaonana hivi karibuni).
United watakutana na Everton tarehe 17 Oktoba, wakati huo huo Ubelgiji na Uholanzi hawajapangwa kukutana hivi karibuni pia, hii inaashiria kuwa Lukaku yuko njiani kuelekea 'OT'.
0 comments:
Post a Comment