Monday, July 6, 2015


David de Gea atarejea kuanza mazoezi kwa ajili ya msimu ujao akitoka Madrid alikokuwa kwenye mapumziko ya likizo.
Golikipa huyo wa Hispania anatarajia kujiunga na Real Madrid kipindi kiki cha majira ya joto baada ya kuwaambia wachezaji wenzake wa Manchester United mpango wake wa kutaka kuondoka Old Trafford.
De Gea ameshindwa kujibu lolote juu ya ofa ya mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki ili asaini mkataba mpya na klabu hiyo Manchester United.
Lakini De Gea aliiambia Cuatro: “Real Madrid? Natakiwa nirudi Manchester United kwa ajili ya mazoezi kabla ya kuanza kwa msimu ujao”, baada ya hapo alikataa kujibu swali jingine lolote lililohusu maisha yake ya baadae.
Van Gaal amepanga kufanya mazungumzo na De Gea juma lijalo ili kujaribu kutafuta suluhu kwa pande zote mbili kwasababu mchezaji huyo yupo kwenye mwaka wake wa mwisho kwenye mkataba wake wa sasa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video