Inafahamika kwamba straika wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo ni mshindani na hapendi kuzidiwa katika maisha yake ya soka.
Sasa stori ni kwamba Ronaldo hapendi kabisa kata kuzidiwa urefu na wenzake wanapopiga picha ya pamoja uwanjani.
Kutokana na hali hiyo, Ronaldo amekuwa akinyenyemea na kusimamia vidole ili awe mrefu au alingane na wachezaji kama Sergio Ramos, Pepe na Tony Kroos ambao hukaa mstari wa kusimama kutokana na vimo vyao.
Mbaya zaidi, Ronaldo amekuwa akimtumia Karim Benzema kama ngazi yake linapofikia suala la kufanya hivyo.
Tazama kwa makini picha zote hapo chini:
0 comments:
Post a Comment