Mbele ya mashabiki 100,000 katika uwanja Melbourne Cricket, Australia kulikuwa na burudani ya aina yake kati ya Manchester City na Real Madrid.
Vijana wa Manuel Pellegrini leo wamekufa 4-1 dhidi ya vijana wa Rafa Benitez.
Mwanasoka bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo ametupia goli moja dakika ya 25, huku Karim Benzema akifunga dakika ya 21, Pepe dakika ya 44 na Denis Cheryshev dakika ya 73 .
Bao la kufutia machozi kwa Manchester City limefungwa dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti na Yaya Toure.
Kuelekea katika mechi hiyo, Toure alisema Man City inahitaji kupunguza pengo lake na Real Madrid pamoja na FC Barcelona katika uwezo wa kusakata kandanda, lakini kwa ushahidi huu pengo limezidi kuwa kubwa.
Ronaldo akiifungia Real Madrid bao baada ya kumzidi maarifa beki wa Man City Aleksandar Kolarov
Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (katikati) akijiandaa kupiga mpira, huku kipa wa Real Madrid, Keylor Navas akiokoa
Toure alikuwa chini ya ulinzi wa Navas na Sergio Ramos
Toure alikuwa na shughuli kali
0 comments:
Post a Comment