Mabingwa wa soka England, Chelsea wameichapa Barcelona kwa penalti 4-2 katika mechi ya International Champions Cup iliyopigwa uwanja wa FedEx Field ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya kwa timu zote.
Mshindi wa mechi hiyo amelazimika kupatikana kwa mikwaju ya penalti kufuatia timu hizo kutoka sare ya 2-2 katika dakika za kawaida.
Katika dakika za kawaida, magoli ya Chelsea yalifungwa na Eden Hazard dakika ya 10 na Gary Cahill dakika ya 86, wakari magoli ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez dakika ya 52 na Sandro dakika ya 66.

WALIOFUNGA NA KUKOSA PENALTI
Iniesta, Barcelona -Alifunga
Falcao, Chelsea- alifunga
Halilovic, Barcelona -aligongesha mwamba
Moses, Chelsea -alifunga
Pique, Barcelona -kipa alidaka
- Ramires, Chelsea -alifunga
Sandro, Barcelona -alifunga
Remy, Chelsea -alifunga
0 comments:
Post a Comment