Nahodha wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ Nadir Haroub ‘Cannavaro’ jana alipewa mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiweka fiti kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ utakaopigwa mwishoni mwa juma hili huko jijini Kampala kwa ajili ya kuwania nafasi ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.
Cannavaro amesema mazoezi hayo maalumu yanatokana na yeye kuwa na jeraha kwenye sehemu yake ya uso lakini leo atakuwa sawa na ataungana na kikosi kizima cha Stars kwa ajili ya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya maandalizi hayo ya kuikabili Uganda.
“Nimepewa mazoezi yangu tofauti kutokana na kwamba, ninamaumivu na natengeneza ufiti wangu ‘special’ kutokana na doctor kuniambia nifanye hivi, nadhani nitaingia na wenzangu kesho (leo) ‘inshallah’ ila kwasasahivi bado natengeneza ufiti”, amesema Cannavaro.
Katika hatua nyingine Cannavaro amesema ujio wa mwalimu mpya (mzawa) Charles Boniface Mkwasa kunaweza kukaiafanya Stars ifanye vizuri kwenye mchezo wa marejeano dhidi ya Uganga kwasababu sasa watatumia mfumo mpya ambao huenda ukawasaidia kufanya vizuri.
“Kwa upande wa wachezaji na benchi la ufundi tunaendelea na mazoezi na wachezaji wanamorali kutokana na kuletwa kwa kocha mpya mzawa ni kocha mzuri na sisi kwa upande wetu tunasikiliza maelekezo wanayotupa kwenye mazoezi”, ameeleza.
Tumebadilika kutokana na kocha Mart Nooij alikuwa anatufundisha mfumo wa 3-5-2, sasahivi kaja Mkwasa tunacheza 4-3-3 inamaana kwamba mfumo unaweza ukatusaidia kwenye mchezo unafuata dhidi ya Uganda”, alimaliza Cannavaro.
0 comments:
Post a Comment