Moja ya viungo wanaotegemewa na Manchester City ni Yaya Toure na uwepo wake uwanjani huifanya timu icheze kwa usalama zaidi, lakini kuna stori mbaya kuhusu mchezaji bora huyu wa Afrika.
Yaya Toure amepandishwa ndege 'Mwewe' kurudi England kwa matibabu zaidi baada ya kuumia katika mechi ya kirafiki iliyopigwa jana , Melbourne, Australia dhidi ya miamba ya kandanda ya Hispania, Real Madrid.
Toure aligongana na golikipa wa Madrid, Keylor Navas ambaye alitoka kwenda kupiga ngumi mpira na Muivory Coast huyo akagongana naye.
Klabu yake imeamua kumrejesha England ili kumtibu kwa umakini, hivyo atakosa mechi za maandalizi ya msimu zitakazopigwa huko Vietnam.
Wakati huo huo, Delph naye alipata majeraha ya nyama za paja katika mechi ya kwanza akiichezea Man City na kutolewa nje kwa machela dakika 20 tu baada ya mechi na inabidi atibiwe haraka kabla ya kuanza msimu mpya.
0 comments:
Post a Comment