Shirikisho la soka nchini TFF limevunja rasmi mkataba wa Ramadhan Singano "Messi' na klabu yake ya Simba baada ya Wekundu hao wa Msimbazi kushindwa kuwasilisha vielelezo mbele ya kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kilichozungumza na mtandao huu, kikao cha kamati hiyo kimemalizika mchana huu na taarifa rasmi inatolewa hivi punde na TFF.
Kutokana na maamuzi hayo, Singano amekuwa mchezaji huru.
Singano alikuwa na mkataba wa miaka miwili ambao alisaini mwaka 2013 na ulitakiwa kumalizika 2015, wakati Simba wao wanadai alikuwa na mkataba wa miaka mitatu ambao Messi alisaini mwaka 2013 na utamalizika 2016.
Bila shaka hizi ni taarifa njema kwa Azam fc ambao wanaiwinda saini ya Singano kwa muda mrefu na kwa maamuzi haya atasajiliwa bure.
0 comments:
Post a Comment