Na Ramadhani Ngoda.
Raisi wa Shirikisho la soka Ulimwenguni, Sepp
Blatter licha ya hivi karibuni kutangaza kuwa atajivua wadhifa huo, ameibuka na
‘kuwachana live’ wote wanaoshikilia kuwa yeye ni miongoni mwa maafisa wa FIFA
waliokula rushwa katika kipindi chake cha uongozi.
Tangu maafisa kadhaa wa FIFA kutuhumiwa kwa rushwa
siku chache kabla ya uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo, kumekuwa na maneno
maneno kuwa uwenda raisi huyo yumo kwenye ‘kapu’ hilo.
Lakini Blatter amekuja juu na kuwataka
wanaomtuhumu kuthibitisha tuhuma zao kabla ya kumtuhumu na sio kuongea kitu
wasichokuwa na ushahidi nacho.
“Watu hawajui neon wanalolitumia wanaponituhumu
kwa rushwa. Mtu anayenituhumu lazima kwanza awe na uthibitisho juu ya hilo”
alisema Blatter.
“Lakini hakuna wa kuthibitisha kuwa mimi ni mla
rushwa kwa sababu sio (mla rushwa). Na atakayesema Blatter ni mla rushwa kwa
sababu tu FIFA ina rushwa, ninachoweza kufanya ni kuwatikisia kichwa tu,”
aliongeza Blatter.
Blatter ameendelea kusisitiza kuwa maneno
yanayosemwa hataraji kama ya athari yoyote katika soka na anachukulia kama
uchafuzi wa maisha yake binafsi.
“Tuhuma hizi juu yangu hazina uhusiano wowote na
soka, ni shambulio kwa maisha yangu binafsi,” alisisitiza raisi huyo.
0 comments:
Post a Comment