Tuesday, July 7, 2015

Klabu ya Simba kupitia msemaji wake Hajji Manara imesema, imepokea taarifa kutoka klabu ya Bidvest Wits FC ya Afrika Kusini alikokwenda Jonas Mkude kufanya majaribio ikisema kwamba, wamemuona mchezaji huyo katika majaribio na wameridhika na majaribio yake.
Afisa habari wa klabu ya Simba Hajji Manara amesema wamepokea barua kutoka klabu ya Bidvest Wits FC ikieleza wameridhishwa na kiwango alichokionesha Mkude na kuahidi kuwa wataendelea kumfatilia huku (Tanzania) aliko ili kuendelea kujua maendeleo yake.
MKUDE2“Jonas Mkude amefanya majaribio, na kwa mujibu wa klabu ile ni kwamba, klabu imetutumia barua kutupa taarifa kuwa imeridhishwa na kiwango chake na wataendelea kumfuatilia huku alipo kwasababu wao walimchukua kwasababu ya ‘trial’ na majibu yake ndio hayo”, amesema Manara.
Majuma kadhaa yaliyopita kiungo wa Simba Jonas Mkude alielekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya majaribio kwenye klabu ya Bidvest Wits ambayo inashiriki ligi kuu ya nchini humo (PSL) lakini haukupita muda mrefu Mkude akarejea jijini Dar es Salaam na badae kujiunga na kikosi cha Simba kilichopo Lushoto kujiandaa na msimu ujao wa ligi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video