Na Ramadhani ngoda.
Kiungo wa kimataifa
wa Algeria na klabu ya Tottenham Hotspur, Nabil Bentaleb hatimaye amefikia
makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka 5 utakaomuweka White hart Lane hadi
mwaka 2020.
Mazungumzo juu ya
mkataba mpya na kiungo huyo almanusra yagonge mwamba msimu uliopita huku
Mualgeria huyo akionesha kuchoshwa na kucheleweshwa kwa hatma yake klabuni hapo
lakini sasa mambo yamekwenda sawa bin sawia na nyota huyo ataendelea kuonekana
akiwa na uzi wa Spurs.
“Klabu inayo furaha
kutangaza kuwa Nabil Bentaleb amesaini mkataba mpya wa miaka 5 utakadumu hadi
2020,” ulisomeka ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa maalum wa twita wa klabu
hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa London.
Bentaleb (20)
amefurahishwa na hatua hiyo na kuashidi kujituma kwa nguvu zake zote awapo
uwanjani ili kufikia malengo ya klabu kwani ndio kinachohitajika kwa mchezaji
aliyethaminuiwa na klabu kwa kupewa mkataba mpya jambo linaloonesha bado
anaaminika na kuthaminiwa.
“Kwa kweli nina
furaha sana kujifunga na klabu hii hadi 2020,” Bentaleb aliiambia tovuti ya
klabu hiyo.
“Klabu imeniamini ni
lazima niwashukuru kwa hilo na kuzidi kuongeza jitihada ili kufikia lengo,”
alisisitiza Bentaleb.
Bentaleb ambaye alikuwa
mchezaji muhimu kwa Spurs msimu wa 2013/14 chini ya aliyekuwa kocha wa timu
hiyo Tim Sherwood, bado anaonekana kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika
kikosi cha kocha Mauricio Pochetino.
0 comments:
Post a Comment