Wednesday, July 15, 2015

Na Simon Chimbo;
Kiungo na nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Bastian Schweinsteiger, wiki hii amekua ni Mjerumani wa kwanza kuichezea klabu ya Manchester United baada ya kusaini mkataba wa miaka 3 akitokea Bayern Munich.
Bastian Schweinsteiger ambaye alipewa jina la 'The Warrior' mara baada ya fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka jana, pia alitungwa jina la 'The Brain' na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew.
Katika fainali ile dhidi ya Argentina, Bastian Schweinsteiger alionesha uwezo mkubwa mno katikati ya kiwanja na kuzima ndoto za Lionel Messi kulitwaa kombe hilo, walilolitwaa Wajerumani kwa ushindi wa goli 1-0.
Mafanikio makubwa aliyoyapata kiungo huyo binafsi, klabuni akiwa na Bayern Munich na hatimaye kutwaa kombe la dunia na timu yake ya taifa ya Ujerumani, yamemuweka Bastian kuwa moja kati ya wachezaji bora wa muda wote duniani.
Bastian ambaye alianza maisha ya soka la kulipwa akiwa na Bayern Munich tangu akiwa na umri wa miaka 18, ameitumikia Bayern kwa kipindi cha miaka 13 huku akishinda mataji yote katika ngazi ya klabu.
Pamoja na kuwa alianza kucheza mpira kama mlinzi wa kushoto alibadilika na kuwa moja kati ya viungo wenye uwezo mkubwa zaidi kupata kutokea ulimwenguni 'commanding midfielder'.
Bastian ambaye kimsingi alianza kujulikana katika ngazi ya soka la kimataifa mwaka 2006 alifanikiwa kuingoza Ujerumani katika fainali za Euro 2008 na kuifikisha fainali walipofungwa na Hispania katika fainali.
Mwaka 2009 Bastian aliungana na kocha Louis Van Gaal mara baada ya kocha huyo kusaini mkataba wa kuifundisha klabu ya Bayern Munich akimpokea Judgen Klinsman.
Alipofika Bayern, Van Gaal alianza kumtumia Bastian kama kiungo wa ulinzi 'defensive midfielder' na kufanikiwa kutwaa makombe mawili huku wakikosa 'treble' walipopoteza katika fainali ya Uefa dhidi ya Internally Milan ya Mourinho mwaka 2010.
Mkosi huo wa klabu bingwa ulaya ulimkuta tena Bastian 2012 walipofungwa kwa mikwaju ya penati na Chelsea ya Roberto Di Matteo katika fainali hiyo ya klabu bingwa.
Hatimaye 2013 katika usiku wa Uefa safari hii ni fainali ya wajerumani wenyewe dhidi ya Borrusia Dortmund katika uwanja wa Wembley, ndipo mikono ya Bastian Schweinsteiger iliposhika kombe la klabu bingwa Ulaya wakishinda 1-0 usiku huo na kumaliza machungu ya kulikosa kwa miaka mingi.
Lakini msimu uliopita ukawa ndio wa mwisho kwa Bastian kuichezea Bayern huku akiinua kombe la ligi kuu Bundesliga na sasa hayupo tena ujerumani.
Bila shaka ni safari ndefu na yenye mafanikio makubwa sana kwa kiungo huyu mpya wa Manchester United hivi sasa. Uzoefu na uongozi wa Bayern ni tunu kwa vijana na mashabiki wa Manchester United katika kipindi hiki watakachokuwa na mjerumani huyu mpiganaji.
Tuzo/Heshima:
World Cup (Germany) - 2014
Club World Cup - 2013
Champions League - 2013
Bundesliga - 2003, 2005, 2006, 2008, 2010, 2013, 2014, 2015
DFB Cup - 2003, 2005, 2006, 2008, 2010, 2013, 2014
DFB League Cup - 2004, 2007
DFL Supercup - 2010, 2012
German Player of the Year - 2013

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video