Na Ramadhani Ngoda.
Mabingwa wa Hispania
na Ulaya, Fc Barcelona hatimaye wameshinda mbio za kuwania saini ya kiungo wa
kimataifa wa Uturuki na klabu ya Atletico Madrid, Arda Turan baada ya
kuthibitisha kumtia mikononi nyota huyo kwa ada ya uhamisho ya Yuro milioni 34
huku ikitarajiwa kupanda hadi kufikia milioni 41 kutokana na vipengele vya
mkataba wake.
Barcelona wanaweza
kumuacha Turan Atletico kama raisi wao ajae ataamua hilo kutokana na kutumikia adhabu
yao ya kutosajili miaka miwili.
Kuemekuwa na tetesi
nyingi juu ya hatma ya Mturuki huyo hasa baada ya kutangaza wazi kuwa
asingeongeza mkataba na Atletico Madrid na vilabu mbalimbali kuibuka kutaka
huduma yake miongoni mwao wakiwepo mabingwa wa Uingereza Chelsea.
Mapema wiki iliyopita
muwania nafasi ya uraisi wa miamba hiyo ya Catalan, Josep Maria Bartomeu
aliweka wazi nia yake ya kutaka kumnasa winga huyo akidai kuwa kocha wa
mabingwa hao Luis Enrique Martinez anamuhitaji kwa udi na uvumba mchezaji huyo.
“Rasmi, Barcelona
inatangaza kumsajili Arda Turan. Karibu Arda,” ulisomeka ujumbe katika ukurasa
wa twita wa klabu hiyo.
Wanaowania uraisi
katika klabu ya Barcelona wamekuwa na ahadi kede kede za kusaini nyota mbalimbali
endapo tu watachaguliwa kuiongoza Barcelona katika uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika Julai 8 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment