Kinda wa Liverpool, Jerome Sinclair anatazamiwa kufuata nyayo za Raheem Sterling baada ya kukataa kuongeza mkataba na klabu yake majira haya ya kiangazi na tayari ameshatweet (picha juu) akionesha dhahiri hana mpango wa kusalia Anfield.
Straika huyo mwenye miaka 18 ambaye hajawahi kucheza timu ya wakubwa ya Liverpool, msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Wigan Atheltic inayoshiriki Championship .
Sinclair aliyesajiliwa kutoka West Brom mwaka 2012 anatarajiwa kuwa moja ya nyota wakubwa wa Liverpool, lakini ndoto za klabu hiyo zinaweza kuyeyuka.
Hapa chini bi baadhi ya Tweets za mashabiki wa Liverpool baada ya kusikia habari za Sinclair kukataa kuongeza mkataba:
0 comments:
Post a Comment