Friday, July 10, 2015

Crystal Palace wamekamilisha usajili wa Yohan Kabaye ambaye amesaini mkataba wa miaka mitatu kukitumikia kikosi hicho akitokea Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

Uhamisho huo unamfanya nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa aungane na kocha wake wa zamani Alan Pardew waliyekuwa pamoja kwenye klabu ya Newcastle United.

Palace watalipa pauni milioni 10 za mwano lakini inaweza kupanda na kufikia pauni milioni 12.8 na kumfanya Cabaye kuwa mchezaji ghali zaidi kununuliwa kwenye historia ya klabu hiyo.

“Nimefurahi kuwa hapa, nilitaka kuja na kucheza hapa kwasababu kuna baadhi ya wachezaji wenye nguvu. Walimaliza vizuri msimu uliopita na nafikiri wanauwezo wa kupambana na kumaliza kwenye nafasi nane za juu”, amesema.

“Pia namfahamu Pardew na nimeshawahi kufanyanae kazi kabla, namuamini”, ameongeza.

“Nataka kufanya vizuri kwa ajili yake kwasababu amefanya jitihada kubwa kunipata na kunileta hapa halikadhalika kwa mwenyekiti, hivyo natoa shukrani zangu za hati kwao”, alimaliza Cabaye.

Ada hiyo ya usajili wa Cabaye inavunja rekodi iliyowekwa na James McAthur aliyesajiliwa kwa pauni milioni saba akitokea Wigan.

‘The Eagles’ wameshinda vita ya kumnasa kiungo huyo ambaye alikuwa akiwaniwa na wakali wa jiji la London klabu ya Tottenham.

Kiungo huyo mchezeshaji wa zamani wa Newcastle United alijiunga na PSG msimu uliopita kwa ada ya pauni milioni 19 lakini amekuwa na wakati mgumu kwa wababe hao wa Ligi 1 akianza kwenye mechi 13 huku akicheza dakika 90 kwenye mchezo mmoja tu kati ya mechi hizo.

Hii ni oroha ya tano bora ya wachezaji walio sajiliwa kwa mkwanja mrefu kwenye historia ya kikosi cha Crystal Palae;
Yohan Cabaye, pauni mlioni 10 (*inaweza kupanda hadi pauni milioni 12.8)
James McArthur, pauni milioni 7
Jordon Mutch, pauni milioni 4.75 (*inaweza kupanda hadi pauni milioni 5.75)
Dwight Gayle, pauni milioni 4.5 (*inaweza kupanda hadi pauni milioni 8.5)
Wilfried Zaha, pauni milioni 3 (*inaweza kupanda hadi pauni milioni 6)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video