Ikitumia kikosi cha vijana wake wa Academy, Azam FC imetoa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar, mchezo ukipigwa kwenye uwanja wa Azam Complex. Mechi hii ilikuwa ya kirafiki.
Azam FC ilikuwa ya kwanza kupata katika dakika ya 27 kupitia kwa Shaaban Idd aliyetengenezewa krosi nzuri na Brien Majwega raia wa Uganda.
Mtibwa iliyoongozwa na nahodha mkongwe, Shaaban Nditi walisawazisha bao hilo dakika ya 38 kupitia kwa Shiza Ramadhani 'Kichuya' aliyewatoka mabeki wa Azam FC akamfanya kipa Mwadin Ally asijue la kufanya.
Kocha mkuu wa Azam, Stewart Hall hakukaa kwenye benchi na badala yake alikuwa jukwaani juu ulipo ubao wa magoli akiufuatilia mchezo huo kwa makini na majukumu akawaachia wasaidizi wake, Idd Cheche na Mario Marineca.
Alisema sababu ya kuwatumia vijana wengi ni kuwapa nafasi na kuwaangalia ili wale wakubwa wapumzike kwa ajili ya mechi ijayo ya Kagame Cup.
Wachezaji wa timu ya wakubwa waliocheza kwa vipindi tofauti leo na kwa sababu maalumu ni Mrundi Didier Kavumbagu, Brian Majwega, Ramadhani Singano 'Messi' na David Mwantika.
0 comments:
Post a Comment