Thursday, July 9, 2015

Kikosi cha ‘wanalambalamba’ Azam FC kinaondoka leo kuelekea jijini Tanga kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la Kagame ambayo inatarajia kuanza juma lijalo jijini Dar es Salaam, wakiwa huko watacheza mechi mbili za kirafiki na African Sports na Coastal Union.
Afisa habari wa Azam FC Jafari Idd amesema, ziara hiyo ina lengo la kukifanyia majaribio kikosi chao baada ya kufanya mazoezi mfululizo chini ya kocha mkuu Stewart Hall.
“Ni kweli Mungu akipenda mchana tunatarajia kuondoka kuelekea Tanga tayari kwa mechi mbili, mechi ya kwanza tutacheza tarehe 11 dhidi ya African Sports tutacheza mchezo mwingine tena dhidi ya Coastal Union”, amesema Idd.
Hiki ni kipindi ambacho mwalimu anaangalia timu jinsi gani ‘performance’ yake inavyokwenda na mchezo wa mpira ni kwamba, mkishafanya mazoezi basi lazima upate michezo ya majaribio kwa ajili ya mwalimu kuweza kuangalia kile ambacho amekifundisha kama kimekuwa ‘achieved’ kwa kiasi gani kwa wachezaji na vilevile kuangalia mambo madogomadogo yaliyojitokeza”, aliongza.
“Kwahiyo timu itasafiri kuelekea Tanga kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Kagame, wachezaji wote wameshafika”, alieleza.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video