Tuesday, July 21, 2015

Matajiri wa jiji la Dar es salaam, Azam FC wameibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini katika mechi ya pili ya kombe la Kagame iliyomalizika jioni hii uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Magoli ya Azam yamefungwa na nahodha mwandamizi wa klabu hiyo, John Raphael Bocco 'Adebayor' katika dakika ya 27' na Kipre Herman Tchetche dakika ya 52.
Hili ni goli la pili la Bocco kwani mechi ya kwanza dhidi ya KCCA ya Uganda, Straika huyo wa Taifa Stars, alifunga goli pekee katika ushindi wa 1-0 kwenye mechi ya ufunguzi ya Kagame Cup iliyopigwa juzi uwanja wa Taifa.
Kwa matokeo hayo, Azam FC wamefikisha pointi sita na kuwa na uhakika wa asilimia 100 kutinga robo fainali. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video