Friday, July 10, 2015

Watanzania tumekuwa watu kusahau sana, na kutokana na hali hii wajanja wachache wametumia mwanya huu wa ujinga wetu kunufaika kirahisi......sisiti kusema Watanzania bado wajinga!
Ukienda kwenye Uchaguzi wa Mgombea wa CCM, mtu ambaye bila kupepesa macho ambaye kila Wizara amefanya kazi, ni John Magufuli lakini angalia jinsi wasahaulifu Watanzania wanavyoaminishwa watu wengine tayari wameshasahau....

Wakati Rage akiwa madarakani, haki ya nani ngonjera za kumkandia zilikuwa nyingi sana na inawezekana hapa labda Watanzania wana maono.

Lakini wapi, najiuliza hivi mbona miaka michache tu ya hawa kina Aveva kuna blunders zaidi ya miaka minne ya Rage!!

Lakini umewahi kuona kuna makala maalumu za kumponda Aveva, je unasikia redioni kina Aveva wanapata vijembe kama vile vya kina Rage??

Sasa labda Aveva anaongoza vizuri Simba, lakini wana Simba wenyewe wanajua kinachotokea na tunaelekea wapi...

Kosa kubwa la Aveva, ambalo namtoa maksi ni yale yale ya kina Dalali, anashindwa kuonyesha U- Rais wake ndani ya Simba, tofauti kabisa na Rage katika himaya yake!

Sitaki kusema Rage alikuwa kiongozi bora, lakini kinachokera kwamba watu huwachukia watu fulani kwa kuwa si watu wao, ila watu wao hata wavurunde vipi wao wako kimya......Bi Hindu leo yuko baraza la Wazee, lakini sijawahi hata siku moja kumsikia akisema chochote kuhusu Simba kana kwamba mambo shwari vile!

Haihitaji akili ya Chuo Kikuu, ukiwekwa na Friends of Simba utaendeshwa nao tu.......:

Phiri alifukuzwa Simba bila Aveva kujua hata kuidhinisha pia....

Tambwe anaachwa pia bila Aveva kujua pia.....

Musoti pia alikatwa bila Aveva kujua pia....

Bila shaka Okwi naye anauzwa bila Aveva kujua pia, kama unabisha, ni hivi Aveva alisema Okwi anaenda majaribio ya siku 14 huko Denmark, siku iliyofuata Hans Poppe anasema Okwi ameuzwa na ada ya uhamisho ni siri, na leo tunaona kweli Okwi amesaini miaka mitano na timu ya Sonderjeskie, sasa hapo utajua nani ni Rais wa timu....?

Na yapo mambo mengi sana Aveva, anakosa sauti nayo, lakini waliompenda ndio wanapenda Rais kama huyu akiambiwa kitu hewala tu, lakini aliyekuwa anakataa kila anachoambiwa ndio yalimkuta yaliyomkuta!

Wakati wa Uchaguzi uliomuingiza Aveva madarakani, nilikuwa napingana sana na upande wa Aveva kwa sababu niliona watu nyuma yake walivyo na hawajawahi kubadilika, lakini kwa kuwa Watanzania ni wasahaulifu na akili za kushikiwa, ndio hivyo wakamchagua!

Sijui ingekuwaje kama Okwi na Messi wanaondoka halafu Rais ndio angekuwa Rage......lakini si magazeti wala redio kuongelea haya wako kimya, watasema nini wakati waliokuwa wanawalipa kumsema Rage ndio wanaharibu sasa!!

Timu iliyoshika nafasi ya tatu, ndio inaachia mastaa wake halafu inategemea wachezaji wapya ndio walete mafanikio.........uwezekano wa kufanikiwa ni mdogo sana kiuhalisia!

Messi na Okwi walikuwa na mchango sana, sasa kina nani wataziba mapengo yao....??

Sina hata chembe ya kumchukia Messi kama wajinga wengine, kwa sababu hawa kina Messi walivumilia sana shida kipindi kina Rage wanaingia madarakani, na bado walitakiwa na timu nyingine lakini wakacheza Simba, najua kuna uhuni walitaka kumfanyia ndio maana naye akaona pamoja na shida alizovumilia halafu bado anatendwa ngoja asepe!

Mchezaji ambaye unamlea inakuwaje unafoji mkataba wake, haya hujafoji kwa nini basi usimpe pesa stahiki, unaanza kutumia ubabe na ujuaji mwingi, hata ungekuwa wewe usingekubali, najua tayari mmesahau ya Hassan Ramadhani 'Kessy'......

Ni uzembe, na upigaji ndio umetawala, yaani wanachafua sana nembo yetu basi, nchi yenyewe imechoka kama watu wake, ngoja tuone ligi ianze tuanze kujipa moyo tena!


I love Simba SC, na sio wanayoiongoza.


Copy and paste kutoka kwa mdau mkubwa wa Simba SC



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video