Monday, July 13, 2015

Mkurugenzi wa michezo wa Inter Milan Piero Ausilio, amethibitisha klabu yake kuwa na mpngo wa kuwasajili Mohamed Salah, Stevan Jovetic na Ivan Perisic - huku akikanusha taarifa zinazowahusisha kumuwania mchezaji wao zamani Zlatan Ibrahimovic na kusema kuwa kwa sasa mchezaji huyo haendani na mipango ya klabu yao.
Wababe hao maarufu kwa jina la Nerazzurri, tayari wameshatumia milioni 40 katika usajili mpaka sasa, ambapo wamefanikiwa kumsajili kiungo Geoffrey Kondogbia kutoka Monaco huku wakifanikiwa pia kumsajili mashambuliaji Jonathan Biabiany bure.
Inter pia wamekuwa wakihusishwa na usajili wa mshambuliaji wa Manchester City Jovetic, mshambuliaji wa Wolfsburg Perisic na winga wa Chelsea Salah huku Ausilio akikiri kuwa kweli wanawafukuzia nyota hao.
Hata hivyo, amekanusha vikali uvumi ulioeneakwamba wanamtaka mshambuliaji nyota wa PSG Ibrahimovic.
"Zlatan ni aina ya wachezaji ambao kwa sasa hawahitaji utambulisho tena lakini pia haendani na programu za klabu yetu", Ausilio aliiambia Runinga ya kalbu.
"Sidhani kama anaweza kuwa sehemu ya mpango wetu... [Jovetic, Perisic na Salah] - hayo ndio majina sasa.
"Kwa upande wa Salah, tunasubiri kwanza kuusoma vizuri muelekeo wake.

13 Jul 2015

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video