Saturday, July 11, 2015


Na Ramadhani ngoda.
Baada ya Mturuki Arda Turan kukamilisha usajili wake kuelekea Fc Barcelona, Atletico Madrid haraka wamemsajili winga wa Kibelgiji anayekipiga kunako klabu ya AS Monaco, Yannick Ferreira Carrasco kama mbadala wake.

Winga huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amesaini mkataba wa miaka 5 na miamba hiyo ya jiji la Madrid baada ya makubaliano ya kukamilisha dili hilo kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 14.3 kufikiwa na pande zote mbili.

Carrasco ambaye mpaka sasa amekwishaichezea timu ya taifa ya Ubelgiji michezo 9, anaoneka kuwa mrithi sahihi wa viatu vilivyoachwa na Arda Turan aliyetimkia Camp Nou hivi karibuni.

“Tumeridhishwa sana na makubaliano yaliyofikiwa kati yetu na Monaco. Kwa sababu Yannick (Carrasco) ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na muelekeo mzuri,” alisema mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid, Jose Luis Perez Caminero baada ya kukamilika usajili huo.

“Anacheza kwa kasi kubwa sana, ni mzuri katika kukokota mpira na ana uwezo mzuri wa kupiga mashuti. Atakuwa na mchango mkubwa sana katika lengo letu na kuongeza ubora wa timu yetu na ushindani pia,” aliongeza Caminero.


Carrasco sasa anakuwa ingizo jipya la tatu Vincente Calderon baada ya kusajiliwa kwa nyota wawili, Jackson Martinez na Luciano Vietto huku mwalimu Diego someone bado akiangalia uwezekano wa kuongeza nyota wengine ili kuboresha kikosi chake kilichokosa ubingwa msimu uliomalizika.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video