Atletico Madrid wamethibitisha usajili wa beki wa kushoto aliyewahi pia kuitumikia klabu hiyo Filipe Luis kutoka Chelsea, ikiwa ni mwaka mmoja tu kupita tangu beki huyo aondoke klabuni hapo.
Luis (29) ambaye amesaini mkataba wa miaka minne, amecheza michezo 26 tu akiwa Chelsea katika michuano yote, akifanikiwa kuchukua kombe la ligi kuu na Capital One, huku akishinhwa kabisa kumtoa mshindani wake Cesar Azpilicueta.
"Timu ya Chelsea leo imefikia makubaliano na klabu ya Atletico Madrid kwa ajili ya uhamisho wa Filipe Luis", imesomeka taarifa kutoka tovuti ya klabu. "Tunamtakia kila la heri katika maisha yake mapya".
Atletico wameripotiwa kutoa kitita cha pauni milioni 11.1 huku wao wakimuuza kwa pauni milioni 15.8 msimu ulipita.
0 comments:
Post a Comment