Hatimaye wakala wa mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema
amethibitisha kuwa uwezekano wa nyota huyo kuihama klabu yake ya Real Madrid na
kujiunga na Arsenal ni jambo la kuchekesha.
Wakala huyo amethibitisha kuwa ana zaidi ya 1000% kwamba Benzema atabakia
klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi.
Taarifa hizo zimekuja kama mkuki ndani ya moyo wa mashabiki wa Gunners
ambao wiki hii yote walikua na matumaini ya kumpata nyota huyo.
Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Olympic Lyon ya Ufaransa, amekuwa
katika headlines kwa muda sasa tangu kuwasili kwa kocha Rafa Benitez kikosini
hapo, ambapo tetesi zimekuwa zikidai huwenda Cristiano Ronaldo akacheza nafasi ya
Karim Benzema, ushambuliaji wa katikati.
Mshambuliaji huyo ambaye ni mfaransa amekuwa akihusishwa sana na kutua
Emirates, lakini kauli hizi za agent wake zinazima ndoto za kocha Arsene Wenger
pamoja na mashabiki kwa ujumla.
Klabu ya Arsenal imekuwa ikikosolewa mara kwa mara kutokana na kukosa
mtu mwenye uwezo wa kufunga na kuwatesa mabeki wa timu pinzani na sasa wanahaha
kutafuta mtu.
Aidha legendari wa klabu hiyo ya Arsenal, Thierry Henry amekua
haridhishwi na uwezo wa mshambuliaji wa sasa wa gunners, Oliver Giroud.
0 comments:
Post a Comment