Mlinda mlango wa Arsenal Wojciech Szczesny yuko mbioni kukamilisha dili la mkopo kwenda klabu ya AS Roma, mtandao wa Goal umethibitisha
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Poland alipoteza nafasi yake ya kikosi cha kwanza kwa David Ospina katika nusu ya pili ya msimu wa ligi kuu nchini Uingereza 2014-2015, licha ya kwamba alicheza mechi 5 kati ya sita ya kombe la FA na kufanikiwa kutetea kombe hilo.
Washika bunduki hao wa jiji la London walimsajili Cech kutoka Chelsea kwa ada ya pauni milioni 11 mapema kabisa, dili ambalo linaonekana kubadilisha kabisa mwelekeo wa Arsenal na kuwa miongoni mwa timu zinazoshindania ubingwa wa EPL.
Wenger sasa ameamua rasmi kuwa Szczesny ataondolewa kikosini kuelekea msimu mpya wa ligi huku Ospina na Damian Martinez wakibakishwa kikosini kuendeleza mapambano na Cech.
Arsene Wenger anaamini kwamba Martinez ,22, bado ana muda mrefu wa kuitumikia klabu hiyo baada ya kumnyakuwa kutoka klabu ya Independence mwaka 2010.
Szczesny sasa atakwenda Roma tayari kuchukua nafasi ya mlinda mlango Morgan De Sanctis ambaye kwa umri wake wa miaka 38, anaonekana kuanza kuchoka huku akiwa amecheza michezo 35 ya ligi msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment