Thursday, July 23, 2015

KOCHA wa Al Khartoum ya Sudan, Kwesi Appiah, amedai kushangazwa na jinsi michuano ya Kombe la Kagame inavyochagua wachezaji bora wa mechi na kudai kuwa ndiyo maana soka la Afrika haliendelei.
Baada ya mchezo wa Al Khartoum na Telecom ya Djibouti kumalizika huku Al Khartoum ikiifunga Telecom mabao 5-0 pale Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kocha huyo ambaye pia aliwahi kuifundisha timu ya Taifa ya Ghana, alilamika kwa benchi lake la ufundi baada ya kuona mchezaji Mohamed Meraneh wa Telecom akitangazwa Mchezaji Bora wa Mechi.
“Ni kichekesho sana, ndio maana soka la Afrika haliendelei. Hata Kagame! Kiukweli inashangaza kuona timu inafungwa 5-0 halafu inatoa mchezaji bora,” alisema.
“Sijui kwa nini inakuwa hivyo, sijui wanatumia kigezo gani kumchagua mchezaji bora wa mchezo.
“Bora wangempa mchezaji bora kama tungetoka sare au kwa utofauti wa mabao yasiyozidi mawili, Lakini mchezaji bora ambaye timu yake imepigwa tano?
“Wenzetu Ulaya wanatushangaa siku zote lakini kumbe hayo yanatokana na sisi wenyewe kutokuwa makini. Nafikiri ni muda sasa tunatakiwa kubadilika na kuacha soka hilo ambalo haliwezi kutupeleka kokote.”
Katika hatua nyingine, kocha huyo ameitangazia vita Yanga watakapocheza kesho kutwa Jumamosi Uwanja wa Taifa.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video