Na Ramadhani Ngoda.
Mchezaji wa
tenisi namba 3 kwa ubora duniani Muingereza Andy Murray amewatoa kimaso maso
Waingereza baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Wimbledon inayoendelea
katika ardhi ya nyumbani kwao kwa kumchapa Mcroatia Ivo Karlovic
kwa seti 7-6 (9-7) 6-4 5-7 6-4.
Murray
(28) licha ya kulinda heshima katika ardhi ya nyumbani, hii kwake ni mara ya 18
mfululizo kutinga robo fainali katika michuano mikubwa ya mchezo huo na sasa atapumzika
siku moja kabla ya kumvaa Mcanada, Vasek Pospisil siku ya Jumatano (Julai 8).
Licha
kushinda mchezo huo, Murray alikiri kupata changamoto kubwa kutoka kwa Mcroatia
huyo na kamwe jaikuwa kazi rahisi kwake kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
“Kiukweli
ilikuwa mechi ngumu sana. Kiakili ilikuwa inachosha kwa sababu inabidi uwe
tayari kwa kila nafasi inayotokea,” alinena Murray baada ya mchezo.
Kikwazo
cha Mrray kutinga nusu fainali ya michuano hiyo kinabaki kuwa ni Vasek Pospisil
aliyemuondosha Muingereza James Ward katika mzunguko wa tatu na baadaye
kumgaragaza Viktor Troicki.
Mzawa
huyo wa Glasgow inambidi kufanya kazi ya ziada kama kweli anahitaji taji hilo
lisitoke nje ya ardhi ya nyumbani yanakofanyikia mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment