Baada ya jana kutia saini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga kwenye klabu ya Azam FC, mshambuliaji wa Kenya Allan Wanga amefunguka juu ya yeye kujiunga na matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.
Wanga amesema kujiunga kwake kwenye kikosi cha Stewart Hall kutaongeza ubora kwenye timu hiyo ambayo mwaka huu itashiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili msimu uliopita.
“Naweza kusema naangalia mbele kuongeza ubora kwenye timu ya Azam, Azam ni timu nzuri imekuwa ikifanya vizuri kwahiyo kujiunga kwangu na Azam naamini kutaongeza ubora wa timu”, amesema Wanga.
Wanga alikuwa anacheza kwenye klabu ya Al Marekh ya Sudan lakini alikataa kuongeza mtaba mpya baada ya mkataba wake kumalizika na kuamua kujiunga na Azam ambao walionesha nia kutaka huduma yake.
Mara baada ya kusaini mkataba, Wanga amerejea nyumbani kwao kwa ajili ya kujiandaa kuja rasmi kuanza kuitumiakia Azam FC kwenye ligi kuu msimu ujao inayotarajia kuanza Septemba 12 pamoja na michuano ya kimataifa ambayo Azam itashiriki.
0 comments:
Post a Comment