Sunday, July 12, 2015


Mshambuliaji Diego Costa wa mabingwa wa soka nchini Uingereza, klabu ya Chelsea amepania kuisaidia klabu yake kwa kufunga magoli mengi zaidi msimu huu.

Diego Costa akiongea na gazeti la daily sunday amesema kama hataathiriwa na majeruhi ya mara kwa mara basi atajitahidi kufunga kila mechi ili kuisaidia Chelsea kutwaa makombe.

Mshambuliaji huyo mwenye asili ya ubabe anapokuwa uwanjani, alifunga magoli 20 ya ligi msimu ulioisha pamoja na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Costa anaeleza kuwa malengo yao kama klabu hayajabadilika. Wanahitaji kuendelea kufanya vizuri zaidi katika ligi za nyumbani huku wakiongeza juhudi zaidi katika michuano ya Ulaya.

Costa anasema, "sisi ni mabingwa wa soka nchini Uingereza lakini tunahitaji kwenda mbali zaidi katika michuano ya ulaya"

Kuhusu nafasi ya Chelsea msimu huu katika ligi, Costa anasema wanahitaji kupigana kwani watapata upinzani mkubwa toka kwa vilabu vingine.


Costa mwenye miaka 26 anaamini klabu za Arsenal, Manchester City, Manchester United na Liverpool zitaleta upinzani mkubwa katika ligi na kwamba wanatakiwa kujipanga.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video