Tuesday, July 28, 2015

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
KLABU ya Al Khartoum imeifanyia kitu mbaya APR FC baada ya kuifumua timu hiyo ya Ligi Kuu ya Rwanda mabao 4-0 katika mechi yao ya leo alasiri.
Mechi hiyo ya robo fainali ya kwanza ya Kombe la Kagame mwaka huu imechezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa kwa mara ya kwanza timu hiyo iliyotinga fainali mbili zilizopita za michuano hiyo, wachezaji wake wakiondoka kwenye uwanja huo kichwa chini.
Mshambuliaji Atif Khalid ndiye aliyepeleka msiba Rwanda baada kufungua akaunti ya mabao dakika ya 11 akimalizia kwa shuti la mguu wa kulia mpira uliookolewa na mabeki baada ya kutokea piga-nikupige ndani ya boksi la maafande hao.
Dakika 11 baadaye mshambuliaji Amin Ibrahim aliipatia Khartoum bao la pili akimalizia kwa shuti kali la mguu wa kulia pasi ya ndani ya boksi iliyosetiwa na mshambuliaji mwenzake Wagdi Awad.
Straika huyo alirejea tena kambani dakika tano kabla ya mapumziko, safari hii akiutendea haki mpira wa pasi murua ya mfungaji wa bao la kwanza, Khalid kwa kupiga shuti lililompita ubavuni beki wa kati wa APR, Rwatubyaye Abdoul baada ya kipa Ndoli Jean kupigwa chenga na mtoa pasi.
APR walijaribi kukaza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko katika kikosi chao wakiwatoa Fiston Nkinzingabo dakika ya 66 na Yannick Mukunzi dakika ya 76 na nafasi zao kuzibwa na Patrick Sibomana na Eric Nsabimana, lakini mabadiliko hayo yalionekana kuwanufaisha wapinzani.
Dakika 10 kabla ya kumalizika kwa mchezo, nahodha wa Al Khartoum, Salh Eldin ambaye jana alianzia benchi kabla ya kuingizwa dakika ya 63 kuchukua nafasi ya Ousmaila Baba, aliipatia timu yake bao la nne likiwa ni la nne pia kwake katika mshindano hayo akimalizia kwa shuti la mguu wa kulia pasi ilyopenyezwa ndani ya sita na mpikaji wa bao la pili, Awad.
Kwa matokeo hayo, Al Khartoum itacheza nusu fainali ya Kombe la Kagame Alhamisi dhidi ya mshindi kati ya mabingwa wa Kenya, Gor Mahia na Malakia FC ya Sudan Kusini ambao jioni ya leo wanacheza mechi ya robo fainali ya pili kwenye Uwanja wa Taifa.  

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video