Saturday, June 6, 2015

Yanga imejiona imelamba dume kwa kumsajili Deus Kaseke aliyemaliza mkataba wake Mbeya City, sasa timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Mbeya, inamsajili Hamis Kiiza.
Kiiza alitamba akiwa na Yanga kabla ya kuachwa mwanzoni mwa msimu uliopita na kisha kutimkia Oman kabla ya kurejea kwao Uganda.

Mmoja wa maofisa wa Mbeya City amelithibitishia Championi Jumamosi kuwa, wapo katika hatua nzuri za kumsajili Kiiza, tayari kwa msimu ujao.

“Kila kitu kinakwenda vizuri na Kiiza anaelekea kusaini mkataba wa kuichezea Mbeya City msimu ujao, tunataka kuimarisha timu baada ya kuondokewa na baadhi ya wachezaji,” alisema bosi huyo mwenye sauti Mbeya City.

Baadhi ya wachezaji walioondoka Mbeya City ni Kaseke aliyejiunga Yanga, Peter Mwalyanzi (Simba), Themi Felix (Kagera Sugar) na Paul Nonga na Anthony Matogolo waliojiunga na Mwadui FC ya Shinyanga.


SOURCE: CHAMPIONI

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video