Patrick Liewig |
Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig amesema yuko tayari kuja kuinoa Mtibwa Sugar kama itakuwa tayari.
Liewig raia wa Ufaransa alikuwa mmoja wa makocha waliokuwa wakiwaniwa na Simba kwa mara nyingine.
Hata hivyo inaonekana nafasi hiyo ameshinda kocha Mwingireza ambaye Simba itamtangaza ndani ya siku chache.
Liewig amekaririwa na Salehjembe akisema: "Kazi yangu ni ukocha, ninaipenda hii kazi pia ninapenda kufanya kazi Tanzania.
"Nimeambiwa Mtibwa Sugar wanatafuta kocha kutoka nje ya Tanzania. Kama nafasi itakuwepo basi nitafurahi na wao watafutahi kwa kazi yangu nzuri."
Mfaransa huyo ni kati ya makocha waliowahi kufanya mabadiliko ndani ya Simba hasa suala la Simba kuamini vijana kwa asilimia kubwa.
0 comments:
Post a Comment