Singano akiwa ametulia nyumbani kwao Keko, Machungwa, Dar es salaam
SHIRIKISHO la soka TanzaniaTFF
limezitaka klabu kushirikiana na SPUTANZA pamoja na Bodi ya Ligi katika kuweka
mifumo mizuri ya uingiaji mikataba.
TFF inao mkataba mama (template) ambao klabu zote na wachezaji wanatakiwa
waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual contracts
between players and clubs).
Hayo yamekuja baada ya kuibuka kwa utata wa mkataba wa
Ramadhan Singano ‘Messi’ na klabu yake ya Simba.
Singano alikuwa na mkataba wa miaka miwili unaoisha mwezi
Julai mwaka huu 2015, wakati Simba wao walikuwa na
mkataba wa miaka mitatu utakaoisha mwezi Julai mwakani.
Katika kikao cha jana ambapo TFF iliwakutanisha Singano na
Simba, pande zote zilieleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo
ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.
Kwa pamoja pande hizo mbili zimekubaliana
kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba mpya utakaoanza
katika msimu mpya wa 2015/16.
Kutokana na maamuzi hayo, Singano ametoa kauli hii: “Wamesema
tukae chini tuongee, mikataba yote haipo, kisheria mimi niko huru” “Tukishindwa
kukubaliana inabidi nitafute timu nyingine, lakini kipau mbele ni kuongea nao
(Simba) kama kweli wana nia au hawana nia na mimi”.
Hata hivyo Singano alitamka bayana kuwa hawezi kuelewana
tena na Simba na hii inaashiria safari ya kutua Azam fc inanukia.
Azam fc wana mpango wa kumsajili Singano endapo utata wa
mkataba wake utamalizika na walishaeleza wazi kuiwania saini yake.
Kikubwa inabidi nipewa mkataba niangalie na kuweka vitu
vyangu. Niwashauri wachezaji wenzangu, bora ukose vitu vyote kuliko kukosa mtu
wa kukuongoza, ukikwama utasaidiwa
0 comments:
Post a Comment