Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
LICHA ya kipigo cha fedheha cha mabao 3-0 dhidi ya Misri yaliyofungwa ndani ya dakika 10, kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, amewaomba Watanzania kutokata tamaa na kipigo hicho.
Stars ilipata kipigo hicho cha nne mfululizo katika mechi za karibuni baada ya kukubali kuianza vibaya safari ya kufuzu Fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Mafarao hao.
Hata hivyo, Nooij amekaririwa na mtandao rasmi wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) leo akieleza kuwa Stars inayo nafasi ya kufuzu AFCON ikiwa haitakata tamaa na kufanya vyema katika mechi zilizobaki.
"Tulicheza vizuri katika nusu ya kwanza ya mchezo, tungeweza kufunga hata mabao mawili. Kosa la kiulinzi likawapa nafasi kutufunga ndani ya kipindi kifupi na walifanikiwa kuumaliza mchezo ndani ya dakika 12. Bado hatujapoteza kitu. Tutaendelea kupambana katika mechi zijazo."amesema Nooij.
Taifa Stars itaikaribisha Nigeria 'Super Eagles' Ijumaa Septemba 9 jijini Dar es Salaam kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza dhidi ya Chad.
0 comments:
Post a Comment