Mchezaji
bora mara nne duniani, Lionel Messi wa FC
Barcelona na timu ya taifa ya Argentina
wiki hii amekuja na kumtetea mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United
na England, Wayne Rooney.
Messi ametoa
kauli ya kumsifia Rooney pale alipoulizwa mtazamo wake wa maneno yanayoenea
chini chini hivi sasa kwamba Uingereza imeshindwa kuzalisha wachezaji wenye
vipaji vya dunia kama mataifa mengine ya Amerika kusini na Uhispania.
Lakini Messi
hakubaliani na mawazo hayo na kudai Uingereza wana wachezaji wenye vipaji na
kusema uwezo wa Wayne Rooney ni mkubwa na anaweza kufananishwa na mchezaji
yeyote yule mwenye uwezo barani Ulaya.
Messi
alisema kiufundi Wayne Rooney ni mchezaji aliyekamilika na kwamba anawazidi
wengi kwa mbali, huku akiongeza kwamba moyo wa Rooney kujituma uwanjani na
kusaidia timu yake ni wa kipekee na mfano wa kuigwa.
Kauli hiy imekuja
wakati mshambuliaji huyo wa Manchester United anakaribia kuvunja rekodi ya
ufungaji bora wa muda wote wa klabu na timu ya taifa.
0 comments:
Post a Comment