KOCHA msaidizi wa Kagera Sugar Mrage Kabange naye amepewa mkono wa kwa heri toka kwa
wakata miwa wa mkoni Kagera baada ya mkataba wake na ‘wana Nkurunkumbi’
kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Kabange
ambaye ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba SC, ameitumikia Kagera Sugar kwa
muda wa miaka nane lakini baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu hakupewa
mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo inayomilikiwa na kiwanda cha
kutengeneza sukari cha Kagera Sugar kilichopo mkoani Kagera.
Winga
huyo wa zamani wa Wekundu wa Msimbazi amesema, milango ipo wazikwa klabu yoyote
inayohitaji huduma yake yeye yupo tayari kufanya nao mazungumzo na kama
watafikia makubaliano basi watafanya kazi pamoja.
“Sina
sehemu yoyote ninayopenda kuelekea, ila milango yangu ipo wazi kwa mtu yeyote
yule ambaye anaona naweza kumsaidia basi aniite tuzungumze halafu tutajua nini
kitaendelea lakini mimi sina mahali popote kusema napendelea kwenda hapa au
pale. Timu yoyote tukayofikia nayo makubaliano mimi nikotayari kufanya nayo
kazi”, amesema Kambange.
“Nawashuhuru
sana Kagera Sugar nimeishi nao kwa wema wale jamaa, hakuna ubaya hata mmoja
wala chuki, sijawahi kugombana na viongozi, wanachama wala wapenzi wa Kagera
Sugar. Nimeishi kwa amani na nimeondoka kwa amani, lakini wao walichosema baada
ya mkataba kumalizika ni kwmba, wanahitaji sura mpya ambayo pengine wanaona
inaweza kuwafikisha mahali pengine kutoka pale ambapo tumeiacha sisi”, Kabange
aliongeza.
“Kwa
mujibu wa katibu wa timu, malengo ya Kagera Sugar yalikuwa ni kumaliza ligi timu
ikiwa kwenye nafasi tatu za juu yaani nafasi ya tatu, ya pili na kuendelea,
sasa sisi hatukuweza kufika katika nafasi hizo”, alimaliza Kambange.
Baada
ya kocha huyo kumalizana na timu yake ya Kagera Sugar, kumekuwepo na taarifa
kwamba Simba SC wanamnyatia kocha huyo ili atue kwenye benchi la ufundi la
Wekundu wa Msimbazi kwa ajili ya kuliongezea nguvu benchi hilo.
0 comments:
Post a Comment