Saturday, June 27, 2015

MABINGWA wa soka Tanzania bara, Young Africans wametoka suluhu na SC Villa ya Uganda 'Jogoo' katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyomalizika usiku huu uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Hata hivyo, Yanga wangeibuka kidedea, lakini katika dakika ya 79' winga wake hatari Saimon Msuva alikosa mkwaju wa penalti uliotokana na kiungo mshambuliaji mpya wa Jangwani, Deus Kaseke kuangushwa na mlinda mlango wa Villa.
Mechi hii ya Hisani ya kuchangia ujenzi wa kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu hususani wenye ulemavu wa ngozi, Albino, ilichelewa kuanza kwa zaidi ya saa moja kwasababu Villa hawakufika uwanjani kwa kile kilichoelezwa kwamba waligoma kutokana na kutolipwa fedha na waandaji wa mechi.
Yanga imewatumia wachezaji wake wapya, Geofrey Mwakiuya, Malimi Busungu na Deus Kaseke, lakini haikuweza kufua dafu mbele ya Jogoo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video